Saturday 26 October 2013

MJADALA NDANI YA JAMII FORUM JUU YA MH. MBOWE

Quote By Haki sawa View Post
Kutokana na mjadala ambao tayari umeshawekwa hapa na kujadiliwa kwa siku mbili mfululizo , nimeona kuwa kuna watu wanafanya propaganda badala ya kujaribu kuutafuta ukweli wa jambo lenyewe na kuangalia rationale ya jambo linalojadiliwa .

Mimi niliamua kufanya jambo moja la kujaribu kuangalia nini alichokua amedeclare Mbowe kwenye Tume ya maadili ya viongozi kwa mujibu wa Sheria ya maadili ya viongozi wa umma , nimekuwa mambo yafuatayo na kama yupo ambaye anaweza kunichallenge na aje a seem hapa na sio kuhangaika na Gutter politics ,

Mbowe Freeman , kwenye fomu zake alideclare kuwa anamiliki nyumba kwenye nchi zifuatazo,USA, UK, SOUTH AFRICA , DUBAI NA NAIROBI . Nyumba zote hizo alionesha alizinunua lini na zipo maeneo gani kwenye nchi hizo ,

Aidha, kuhusu kumiliki Akounti ya Benki nje ya Nchi alionesha kuwa anamiliki Akaunti iliyopo London Barclays Bank na nyingine iko Hull City, na Benki moja USA .Ila hana Akaunti katika nchi ya Uswisi wala kwenye offshore nyingine zozote zile .

vyote hivyo vipo kwenye fomu ya maadili ya viongozi , pia alionesha kuwa Ana madeni kwenye mabenki mbalimbali ndani nanje ya nchi , na hii ni kwa mujibu wa sheria .

Sasa hapo nimeona nisaidie kutoa ufafanuzi huu, na kama mtu unataka unaweza kwenda pale tume ya maadili ya viongozi wa umma na unalipia kiasi cha shilingi 1,000 tu na unapewa fomu hizo ila huruhusiwi kuondoka nazo wala kupiga picha au kutoa nakala ya fomu (photocopy) .

hivyo , jukwaa kuendelea na kujadiliana kuhusu nyumba moja ya DUBAI , ni vyema jukwaa likarudi kwenye heshima yake ya siku za nyuma ya kuwa mbele ya waandishi kwa kwenda hatua moja mbele katika kuutafuta ukweli wenyewe na sio kuendelea kulifanya jukwaa kuwa kama sehemu ya udaku.

Hivyo, basi badala ya kusubiria wakina Ezekiel Kimwaga , kuandika taarifa za upande mmoja wanaotaka wao kuwa ni Mbowe, Rostam Na Ngeleja tu ndio ambao waliombwa kusaidia timu hiyo katika kutafuta ukweli wa fedha za Uswisi, ni kuwa wabunge wote walioongea siku ya mjadala huo walihojiwa akiwemo Zitto Kabwe ambaye alihojiwa kwa saa nane na timu hiyo, pamoja na wabunge wengine wengi na wafanyabiashara wakiwemo mameneja wa Benki mbalimbali na wamiliki wa maduka ya fedha .

Ni Imani yangu kuwa kwa hili nimeweza kulisaidia jukwaa kuwa na mjadala ambao ni focused , na turejee historia yetu ya kubwa mbele ya media nyingine na sio kama ambavyo leo tunakuwa .........
  Fuatilia zaidi: http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/542854-freeman-mbowe-anamiliki-jumba-la-kifahari-dubai.html

SOURCE: JAMII FORUM